28 Agosti 2026 - 22:34
Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum Apewa Hati ya Ushindi, Aaminiwa Tena Kuongoza JMAT-Taifa

Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum ameibuka mshindi katika uchaguzi wa JMAT Taifa na kukabidhiwa rasmi Hati ya Ushindi mjini Dodoma - Tanzania, akipewa dhamana ya kuendelea kuongoza Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) kwa kipindi kingine.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA-, Tume ya Uchaguzi ya Jumuiya ya Maridhiano na Kamati za Amani Tanzania (JMAT) imemkabidhi rasmi Hati ya Ushindi Mwenyekiti wa JMAT Taifa, Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum, baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa uongozi wa jumuiya hiyo.

Hati hiyo ya ushindi imekabidhiwa tarehe 27 Agosti 2026, mjini Dodoma - Tanzania, ikiwa ni uthibitisho wa kuaminiwa tena kwa Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum kuendelea kuiongoza JMAT Taifa kwa kipindi kingine.

Ushindi huo umetajwa kuwa ni kielelezo cha imani, heshima, uaminifu na matumaini makubwa ambayo wajumbe wa JMAT wameendelea kuwa nayo katika uongozi wa Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum.

Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum Apewa Hati ya Ushindi, Aaminiwa Tena Kuongoza JMAT-Taifa

Katika kipindi chake cha uongozi, Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum ameendelea kuonesha uwezo wa kuunganisha watu, kujenga maridhiano, kusimamia taasisi na kutafuta suluhu katika masuala mbalimbali yanayohusu jamii.

Aidha, uongozi wake umejikita katika kuimarisha umoja na mshikamano, pamoja na kusukuma mbele agenda za maendeleo ya JMAT na kukuza ushirikiano miongoni mwa maimamu, wanazuoni na viongozi wa dini.

Uzoefu wake wa kiuongozi na nafasi yake katika jamii umeendelea kumjengea heshima na kuaminika miongoni mwa viongozi, wanazuoni, Maimamu na Waumini.

Kukabidhiwa kwa Hati ya Ushindi tarehe 27 Agosti 2026 mjini Dodoma kunafungua ukurasa mpya wa uongozi wa JMAT Taifa, huku dhamana hiyo mpya ikiambatana na matarajio ya kuendeleza umoja, mshikamano, elimu, ustawi wa maimamu na wanazuoni, pamoja na kuimarisha mchango wa JMAT katika kujenga jamii yenye amani, maadili na maendeleo.

Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum Apewa Hati ya Ushindi, Aaminiwa Tena Kuongoza JMAT-Taifa

Kwa upande mwingine, Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum ametakiwa kutumia dhamana hiyo mpya kwa hekima, uadilifu na weledi, huku akipewa pongezi kwa kuaminiwa tena kuiongoza JMAT Taifa.

Ushindi huo umetajwa kuwa si ushindi wa mtu binafsi pekee, bali ni ushindi wa JMAT, maimamu na wanazuoni, pamoja na ishara ya imani ambayo wajumbe wameendelea kuiweka katika uongozi wake.

Wadau wamemuombea Mwenyezi Mungu amjalie hekima, afya, nguvu na uwezo wa kuibeba dhamana hiyo kwa uadilifu na mafanikio.
Uongozi ni dhamana; ushindi ni mwanzo wa kazi.

Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum Apewa Hati ya Ushindi, Aaminiwa Tena Kuongoza JMAT-Taifa

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha